Samia:Tutaendeleza mema ya Magufuli

Muktasari:

  • Rais Samia Suluhu Hassan amesema mema yote yaliyoachwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli yataendelezwa


Chato. Rais Samia Suluhu Hassan amesema mema yote yaliyoachwa na aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli yataendelezwa

Ameyasema hayo leo Alhamisi Machi 17, 2022 alipokuwa akitoa salamu za taifa katika maadhimisho ya mwaka mmoja wa kumbukizi ya kifo cha hayati Magufuli.

Rais Samia ameyataja mambo hayo kuwa ni pamoja na nidhamu, uadilifu na kupiga vita ubadhilifu.

"Hivi karibuni tutafungua daraja la Tanzanite lililoko jijini Dar es salaam hii ilikua ndoto ya Magufuli na nitaiendeleza kwa kuboresha huduma za maji, umeme na miundombinu"amesema Samia

Akizungumzia miradi iliyopo Geita, Rais Samia amesema mradi wa kivuko cha Chato-Nkome kilichogharimu Sh3.1 bilioni umekamilika.

Aidha mradi wa kituo kikuu cha mabasi unaojengwa kwa Sh13.2 bilioni umekamilika kwa asilimia 92 na kuahidi kuendelea kutoa fedha ili ukamilike kwa asilimia 100

Samia amesema mambo yote hayo yatawezekana kama watanzania wataendelea kuimarisha mshikamano.

"Sisi wanadamu hatuwezi lolote bila msaada wa mwenyezi Mungu"

Awali Makamu wa Rais wa Tanzania, Philip Mpango amesema Magufuli alikua mwalimu wake aliyemfundisha kumtegemea Mungu nyakati za shida.

Exclusive: Mahojiano maalumu na Rais Samia Suluhu Hassan

Rais Samia Suluhu Hassan anatimiza mwaka mmoja tangu achukue madaraka ya nchi, pamoja na maendeleo aliyoyasimamia amebainisha mikakati yake muhimu katika kuijenga nchi. Soma zaidi