Songwe yavuka lengo chanjo ya polio Jumla ya watoto 282,000 wenye umri chini ya miaka mitano mkoani Songwe wamepata chanjo ya kujikinga na ugonjwa wa polio katika kipindi cha kampeni maalumu ya siku nne.
Magari mawili yatelekezwa yakiwa na bidhaa za magendo Magari mawili yaliyokuwa yanasafirisha bidhaa za magendo kutoka Tunduma kuelekea Mbeya yamekamatwa katika mji wa Vwawa wilayani Mbozi mkoani Songwe yakiwa yametelekezwa, baada ya moja aina ya...
Wakamatwa kwa kuazimisha silaha kwa watuhumiwa wa ujambazi Watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuazimisha silaha kwa mtuhumiwa wa ujambazi.
Watatu wa familia moja wafa wakiwa wamelala Watu watatu wa familia moja akiwamo mama mjamzito wamefariki dunia baada ya gema la udongo kuporomoka na kuangukia nyumba waliyokuwa wamelala wilayani Ileje, Mkoa wa Songwe.
Daladala zagoma Songwe, abiria wahaha Madereva wa daladala zinazofanya safari kati ya Mlowo na Tunduma mkoani Songwe wamesitisha huduma za usafirishaji wa abiria wakidai wanasubiri tamko la Serikali la kupandisha nauli.
Wawili wakamatwa wakisafirisha wahamiaji haramu 20 Madereva wawili wa malori yaliyokuwa yakitoka Dar es Salaam kwenda DRC Congo wamekamatwa mkoani Songwe baada ya kukutwa wakiwasafirisha wahamiaji haramu 20 kutoka Somalia na Ethiopia.
Michezo ya ‘PS’ yawaliza wazazi Wadau mbalimbali wametaka michezo ya mitandaoni inayochezwa mitaani maarufu kama ‘Play Stations’ (PS) ipigwe marufuku kwa watoto au kupangiwa muda maalumu.
Wanne wafa, 35 wajeruhiwa ajali ya basi Songwe Watu wanne wamefariki na wengine 35 wemejeruhiwa baada ya basi la Kilimanjaro Express kupata ajali eneo la Senjele wilayani Mbozi Mkoa wa Songwe.
Basi lapata ajali Songwe Basi la kampuni ya Kilimanjaro linalofanya safari kutoka Tunduma kwenda Dar es Salaam limepata ajali maeneo ya Senjele mkoani Songwe.
Wawili wafariki magari yakigongana na kuwaka moto Mbozi Watu wawili wamefariki na wengine watatu kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili likiwamo lililobeba mafuta na kuwaka moto katika ajali iliyotokea maeneo ya Old Vwawa wilayani Mbozi...